Monday, 21 March 2016

Zanzibar Amani Milingitini Sports Fans


AMANI MILINGOTINI SPORTS FANS


UTANGULIZI

 Zanzibar ni chimbuko la mambo mengi ya kimichezo hapa Afrika ya Mashariki. MicheMawa  hapa visiswani kabla hata haijajulikana barani Afrika. Michezo ya awali ni pamoja na football. Golf, Cricket, Kuogelea, tenis, Mchezo wa Ng’ombe  na kadhalika. Ilifika wakati Zanzibar ilikuwa juu katika medani za soka hasa wakati wa Gossage. Tunafahami kuwa michezo na wana-Michezo ni muhimu katika kutoa mchango wa kiafya, mahusiano ya kimataifa na uchumi wa Taifa.  Hata hivyo,  oeo hii michezo imefifia.  Jumuiya hii inalenga katika kuwakusanya na kuwaleta pamoja wana-Michezo mbali mbali katika kupenda na kuinua viwango vya michezo na hasa soccer ili kuinua viwango na kuwapatia ajira wapenzi na wachezaji wa hapa Zanzibar.

 

1) Jina la Jumuiya

Jina la Jumuiya hii ni “Wapenzi wa Michezo – Amani Milingotini. Kwa Kiingereza ni “Amani Milingotini Sports Fans” kwa kifupi  (AMSF).

 


2) Ofisi za Jumuiya

Makao Makuu ya Jumuiya yatakuwa Amani Milingotini na anwani ya Posta itakuwa ni P.O. Box 4752, Zanzibar. Email: AmaniSoccerFuns@yahoo.com

 
3) Hadhi

Jumuiya baada ya kupata usajili rasmi itakuwa ni chama chenye
 i) (a) nguvu na hadhi kisheria na itakuwa na uwezo wa kushitaki na kushitakiwa
(b)   kumiliki mali, kuingia katika mikataba, kuuza, kununua, kukodi na kukodisha
(c)    kutoa kwa njia yoyote ile mali kwa jina la Jumuiya  kwa mujibu wa sheria za nchi

 


ii) Jumuiya hii itakuwa ni Jumuiya ya hiari na isisiyokuwa wa ya kidini, kiserikali wala ya kisiasa na ni Jumuiya isiyokuwa na malengo ya kugawana faida miongoni mwa wanachama wake

 
 
3)  Malengo makuu ya Jumuiya

                    i.            Jumuiya hii inalenga katika kuwakusanya na kuwaleta pamoja wapenzi na wana-Michezo Zanzibar.

                  ii.            Kuinua mapenzi na hamasa za kimichezo mbali mbali  ili kuinua viwango vya michezo na hasa soccer ili kukuza soko la  ajira kwa vijana wa Zanzibar.
                iii.            Kuanzisha mfuko wa michezo kwa lengo la kusadia wanamichezo kitaaluma
                iv.            Kushirkiana na wadau wa nje na ndani ya nchi katika kukuza michezo
                  v.            Kuelimisha na kutoa miongozo kwa wanamichezo na wanachama wa Jumuiya
                vi.            Kutafuta nyenzo za kazi zikiwemo fedha ,utalaam na vifaa
              vii.            Kuanzisha miradi ambayo itasadia kuinua maisha ya jamii

   
   
 4.0)  Uanachama
4.1 Aina za Uanachama 

Jumiya itakuwa na wanachama wa aina tatu, nazo ni:

i)           Wanachama  Waanzilishi
ii)      Mwanachama wa kawaida na
iii)  Mwanachama kutunukiwa/maalum

   
   
 
5.2) Sifa za kuwa mwanachama

i)                    Waanzilishi: Hawa ni wanachama walioanzisha Jumuiya ambao nao watatakiwa kuwa wanamichezo, wapenzi wa michezo mradi na awe amefikia umri wa miaka 18 au zaidi na akili timamu.
 
ii)                  Mwanachama wa kawaida: Anaweza kuwa mtu yoyote ambae mkaazi wa Unguja Zanzibar ambae ana taaluma ya Michezo na awe amefikia umri wa miaka 18 au zaidi na akili timamu.

iii)     Mwanachama kutunukiwa: Mtu yeyote mwenye umri wa miaka 18 au zaidi na mwenye akili timamu ambae ana mapenzi na taaluma ya michrzo hasa soka kutoka sehemu yoyote ya Dunia anaweza kupewa uanachama huu baada ya kamati tendaji kuona anafaa.

    
 6.0)     Jinsi ya kuwa mwanachama

i)        Mtu yoyote anaetaka kuwa mwanachama wa AMSF atatakiwa kujaza fomu ya maombi ambayo itauzwa kwa mujibu wa taratibu zitazopangwa na Kamati Tendaji. Kamati Tendaji itajadili ombi na muombaji na atajulishwa katika kipindi kisichozidi miezi miwili kuanzia tarehe yake ya maombi. Kwa yule ambae hatokubaliwa atarudishiwa fedha zake ambazo zitakatwa robo yake kufidia gharama za kiuendeshaji.

 ii)   Wanachama waanzilishi pia watajaza na kulipa fomu hii ya kujiunga na Jumuiya
 



 
 ++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
 
Contacts persons
Mr. Isa Ahmada
 
Mr. Yussuf H Kombo
  +255 713 459447; Email: yhkombo@yahoo.com
 
Hassan