AMANI
MILINGOTINI SPORTS FANS
UTANGULIZI
Jina la Jumuiya hii ni “Wapenzi wa Michezo – Amani Milingotini.
Kwa Kiingereza ni “Amani
Milingotini Sports Fans” kwa kifupi (AMSF).
2) Ofisi za Jumuiya
Makao Makuu ya Jumuiya yatakuwa Amani Milingotini na anwani
ya Posta itakuwa ni P.O. Box 4752, Zanzibar. Email: AmaniSoccerFuns@yahoo.com
3) Hadhi
Jumuiya baada ya kupata usajili rasmi itakuwa ni chama chenye
i) (a) nguvu na hadhi
kisheria na itakuwa na uwezo wa kushitaki na kushitakiwa(b) kumiliki mali, kuingia katika mikataba, kuuza, kununua, kukodi na kukodisha
(c) kutoa kwa njia yoyote ile mali kwa jina la Jumuiya kwa mujibu wa sheria za nchi
ii) Jumuiya hii itakuwa ni Jumuiya ya hiari na isisiyokuwa wa
ya kidini, kiserikali wala ya kisiasa na ni Jumuiya isiyokuwa na malengo ya
kugawana faida miongoni mwa wanachama wake
i.
Jumuiya hii inalenga katika kuwakusanya na kuwaleta pamoja wapenzi
na wana-Michezo Zanzibar.
ii.
Kuinua mapenzi na hamasa za kimichezo mbali mbali ili kuinua viwango vya michezo na hasa soccer
ili kukuza soko la ajira kwa vijana wa
Zanzibar.
iii.
Kuanzisha mfuko wa michezo kwa lengo la kusadia wanamichezo
kitaalumaiv. Kushirkiana na wadau wa nje na ndani ya nchi katika kukuza michezo
v. Kuelimisha na kutoa miongozo kwa wanamichezo na wanachama wa Jumuiya
vi. Kutafuta nyenzo za kazi zikiwemo fedha ,utalaam na vifaa
vii. Kuanzisha miradi ambayo itasadia kuinua maisha ya jamii
4.1 Aina za Uanachama
Jumiya itakuwa
na wanachama wa aina tatu, nazo ni:
i)
Wanachama Waanzilishi ii) Mwanachama wa kawaida na
iii) Mwanachama kutunukiwa/maalum
5.2)
Sifa za kuwa mwanachama
i)
Waanzilishi: Hawa ni wanachama walioanzisha
Jumuiya ambao nao watatakiwa kuwa wanamichezo, wapenzi wa michezo mradi
na awe amefikia umri wa miaka 18 au zaidi na akili timamu.
iii) Mwanachama kutunukiwa: Mtu yeyote mwenye umri wa miaka 18 au zaidi na mwenye akili timamu ambae ana mapenzi na taaluma ya michrzo hasa soka kutoka sehemu yoyote ya Dunia anaweza kupewa uanachama huu baada ya kamati tendaji kuona anafaa.
i)
Mtu
yoyote anaetaka kuwa mwanachama wa AMSF atatakiwa kujaza fomu ya maombi ambayo
itauzwa kwa mujibu wa taratibu zitazopangwa na Kamati Tendaji. Kamati Tendaji
itajadili ombi na muombaji na atajulishwa katika kipindi kisichozidi miezi miwili
kuanzia tarehe yake ya maombi. Kwa yule ambae hatokubaliwa atarudishiwa fedha
zake ambazo zitakatwa robo yake kufidia gharama za kiuendeshaji.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Contacts persons
Mr. Isa Ahmada
Hassan





































No comments:
Post a Comment